Kipindi hiki ilikuwa nafasi ya washiriki kufanya tathmini ya maandalizi ya uchaguzi unaotegemea kuanza hapo mwezi Mei mwaka huu wa 2010. Maandalizi hayo yalianzia katika ugawaji wa vitambulisho kwa raia ambao hawakuwa navyo, shughuli ambayo ilifuatwa na uandikishaji wa wapiga kura ulioanza rasmi tarehe 21 Januari 2010.